Hawa ndio wasichana 3 warembo waliokamatwa kwa ‘kutwerk’hadharani na kuonesha sehemu zao za siri

Wasichana watatu wa Oregon, Marekani wamekamatwa na polisi Jumatatu hii kwa kutwerk (kukatika kwa kutingisha makalio) hadharani na kuwatamanisha wanaume kimapenzi.


Coura Velazquez, Brittany Medak na Leokham Yothsombath waliokamatwa na polisi
Kama haitoshi, wasichana hao walionesha pia nyeti zao ambapo mmoja alibinua sketi yake na kutanua miguu katikati a magari mawili kuonesha sehemu hizo. Mmoja wa wanawake hao, Leokham Yothsombath alionekana akirekodi tukio hilo kwenye simu. Video hizo azijasambaa Youtube kwakuwa walikamatwa na polisi na kukutwa pia na madawa ya kulevya.
Wasichana hao ni Coura Velazquez, Brittany Medak na Leokham Yothsombath. Polisi wa Beaverton wamesema kuwa Coura Velazquez alienda kwenye mahakama ya manispaa kulipa faini na yeye na marafiki zake wawili walipoondoka kwenye jengo hilo walianza kukatika mbele ya mahakama hiyo huku watu wengi wakishuhudia. Velazquez na Brittney Medak, ambao wote wanatokea Vancouver, walionesha nyeti zao wakati wakitwerk na Medak alinyanyua sketi na kujisaidia haja ndogo katikati ya magari mawili.
Watatu hao walipanda kwenye gari la Medak na kukimbia japo hawakufika mbali kabla ya kukamatwa na polisi. Ndani ya gari polisi walikuta bangi, cocaine na madawa mengine. Wanakabiliwa na makosa mengi na bado wapo polisi.
Previous Post Next Post

Popular Items