Dr Dre kuwa billionaire wa kwanza mwana hip hop, apple yanunua kampuni yake kwa dola billion 3, Diddy akubali kufunikwa

Kampuni ya Apple imepanga kuinunua kampuni ya Dr. Dre ya ‘Beats Electronics’ inayotengeneza bidhaa ya headphones maarufu za ‘Beats by Dr Dre’ na imepanga kumlipa dola billion 3.



Malipo hayo yatamfanya Dr Dre kuwa sio tu mwanamuziki tajiri zaidi duniani lakini pia mwanahip hop wa kwanza kuwa Billionaire.

Kwa mujibu wa Finance Times, endapo Apple watanunua kampuni hiyo kwa dola billion 3.2 itakuwa imefanya manunuzi yenye thamani zaidi ya kuinunua kampuni nyingine.

Mchongo huu utamfanya Dr. Dre kuupiku utajiri wa P.Diddy ($ 700 Million) zaidi ya mara tatu kwa kuzingatia kuwa Diddy ndiye rapper mwenye pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa akifuatiwa na Dr Dre kwa mujibu wa Forbes.

Kupitia Instagram, Puff Daddy ameandika ujumbe wa kumpongeza Dr Dre na kuonesha kuwa sasa inabidi aongeze bidii ‘time to go to work’.

“This is BIG! This is Historical! If anyone deserves it, it's you! Congratulations Dr. Dre! #fromthesoontobe #DrCombs #wemadeit #proudofyou #thebarhasbeenrsised #motivated #timetogotowork.” Puff Daddy ameandika kwenye Instagram na kuambatanisha picha ya Dr Dre..
Previous Post Next Post