Donald Sterling akataa kulipa fidia ya $2.5 milion kwa kosa la ubaguzi wa rangi, atishia kuishitaki NBA

Donald Sterling ambaye ni mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Clippers amekataa kulipa fidia iliyoamriwa na NBA kwa kosa la kufanya ubaguzi wa rangi wakati akiongea na mpenzi wake.

USA Today imeripoti kuwa mwanasheria wa mzee huyo tajiri, Maxwell Blecher alimtumia barua makamu wa raisi wa NBA Rick Buchanan akieleza kuwa bwana Donald Sterling hajafanya kosa lolote na kwamba hasitahili adhabu yoyote.



Donald Sterling mwenye umri wa miaka 80 alikubwa na kashfa nzito baada ya maongezi yake na mpenzi wake yaliyojaa ubaguzi wa rangi kuwekwa kwenye mtandao maarufu wa udaku ‘TMZ’.

Bwana Donald alipofanya mahojiano na CNN alieleza kuwa anaamini kabisa kuwa mpenzi wake alimtengenezea mtego ili afanye kosa hilo kubwa kwa kuwa hata yeye wakati anasikiliza tena maongezi hayo hakuelewa ni kwa nini alizungumza yote yale.

Kitendo chake kililaaniwa na watu mbalimbali huku baadhi yao wakitangaza nia ya kuinunua Clippers.

Previous Post Next Post

Popular Items