Diddy ataka kuinunua LA Clippers kwa gharama yoyote, Floyd Mayweather pia aonesha nia

Baada ya shirikisho la mpira wa kikapu nchini marekani NBA kumfungia maisha mmiliki wa timu ya LA Clippers, m Donald sterling baada ya kupatikana na hatia ya ubaguzi, watu maarufu wameonesha nia ya kuinunua timu hiyo akiwemo Rapper na mfanyabiashara Diddy.


Diddy ameonesha nia ya kutaka kuinunua timu hiyo ya mpira wa kikapu kwa gharama yeyote.

"I will always be a Knicks fan, but I am a business man. #DiddyBuyTheClippers #NameYourPrice" inasomeka tweet ya Diddy .

Mtu mwingine alionesha nia ya kutaka kununua timu hiyo ni bondia Floyd Mayweather na muigizaji Frankie Muniz.

Floyd alionesha nia yake wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu pambano lake lijalo dhidi ya Marcos Maidana na alipendekeza rafiki zake ambao ni mabillionaire kuweka pesa mezani washindanie kuinunua timu hiyo.

LA Clippers kwasasa inakadiliwa kuwa na dhamani ya dola milioni 575.

Hata hivyo, Donald Sterling hajaonesha nia ya kuiuza timu hiyo maarufu ya kikapu.
Previous Post Next Post