Mmiliki wa timu ya L.A Clippers, Donald Sterling afungiwa maisha kushiriki NBA

Mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Clippers, Donald Sterling amepigwa marufuku na chama cha mchezo huo, NBA katika maisha yake kujihusisha na mchezo huo pamoja na kupigwa faini ya dola milioni 2.5 kufuatia kauli ya kibaguzi wa rangi aliyoitoa kwenye mazungumzo yake na mpenzi wake wa zamani V. Stiviano.




Donald Sterling na mpenzi wake V. Stivian

Kamishina wa NBA, Adam Silver ametangaza adhabu hiyo jana wakati akiongea na waandishi wa habari.

Makampuni mengi yamejiondoa kama wadhamini kwenye timu ya kikapu Los Angeles Clippers kufuatia kauli ya kibaguzi iliyotolewa na mmiliki wa timu hiyo, Donald Sterling dhidi ya Wamarekani weusi. Makampuni hayo ni pamoja na CarMax, State Farm Insurance, Kia Motors America, Virgin America, maji ya P. Diddy, AQUAHydrate, Red Bull, Yokohama tires na Mercedes-Benz. Red Bull imejiondoa kuisaidia Clippers lakini itaendelea kumdhamini



Mazungumzo hayo yaliwekwa kwenye mtandao wa TMZ ambapo Sterling anamkaripia Stiviano kwa kuwa karibu na watu weusi na kwa kupost picha kwenye Instagram akiwa na mchezaji wa zamani wa Lakers, Magic Johnson.
Maneno aliyosema ni pamoja na: “It bothers me a lot that you want to broadcast that you’re associating with black people. Do you have to? You can sleep with [black people]. You can bring them in, you can do whatever you want. The little I ask you is not to promote it on that … and not to bring them to my games.”
Previous Post Next Post

Popular Items