Video: 'The Ultimate Warrior' afariki baada ya kuanguka ghafla, Ni Mcheza mieleka maarufu

Mcheza mieleka maarufu aliyetumia jina la The Ultimate Warrior amefariki Jana (April 8) akiwa na umri wa miaka 54, ikiwa ni siku chache baada ya kupewa heshima kwa kuingizwa kwenye WWE Hall of Fame.



WWE imethibitisha kifo chake kupitia website yao na kuandika ujumbe kuonesha jinsi walivyoguswa na msiba huo.

“WWE is shocked and deeply saddened to learn of the passing of one of the most iconic WWE Superstars ever, The Ultimate Warrior. WWE sends its sincere condolences to Warrior's family, friends and fans." Wameandika WWE

Tazama video hapa chini



Kwa mujibu wa TMZ, mcheza mieleka huyo alipoteza maisha katika eneo la hotel huko Arizona majira ya saa kumi na moja jioni baada ya kuanguka ghafla wakati yeye na mkewe wakitembea kuelekea kwenye gari lao.
Previous Post Next Post