Video: Jose Mourinho atangaza vita kali kwa PSG

Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameonyesha kuwa na uhakika wa kikosi chake kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambapo hii leo kitakuwa na shughuli pevu ya kuwakabili mabingwa wa soka kutoka nchini Ufaransa Paris Saint German katika mchezo wa mkondo wa pii wa hatua ya robo fainali utakaochezwa Stamford Bridge.

Mourinho ameonyesha kujiamini huko kufutia majibu aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari ambao walimuuliza kama ana uhakika wa kufanya maajabu ya kuwaondoa PSG kwenye michuano hiyo baada ya kikosi chake kukubali kisago cha mabao matatu kwa moja katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa juma lililopita huko Park De Princes huko jijini Paris.



Mourinho amesema hafikirii kushindwa katika mchezo wa hii leo, kwani walicho nacho wapinzani wao kutoka nchini Ufaransa na wao kama Chelsea wanacho hivyo haoni sababu ya kujikatisha tamaa ili hali kuna mchezo wa mkondo wa pili ambao utaweza kutoa nafasi kubwa kwa upande wa The Blues.






Mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali utachezwa nchini Ujerumani katika mji wa Dortmund ambapo magwiji wa soka kutoka nchini Hispania Real Madrid watakua na kibarua cha kuwakabili wenyeji Borussia Dortmund katika uwanja wa Signal Iduna Park hii leo.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliozikutanisha klabu hizo, ilishuhudiwa Borussia Dortmund wakikubali kichapo cha mabao matatu kwa sifuri, hivyo itawalazimu wajerumani hao kusaka zaidi ya mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa hii leo.
Previous Post Next Post

Popular Items