Dully Sykes aeleza moja kati ya siri ya mafanikio ya Diamond

Jina la Diamond Platinumz mtoto wa Tandale mwenye historia ya kuishi maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya majina makubwa kimuziki barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama One Campaign iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa Afrika Magharibi.

Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.

“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully Sykes.



Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.

Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.

“Kama wangekuwa wajanja sasa hivi wangekuwa na vitega uchumi…kitu kama studio ni kama jiko. Unakula kwa kutumia studio. Hata kama mtu haji lakini unaweza kutengeneza muziki kwa kutumia akili yako ukasema ‘leo bwana nimeamka saa kumi ya usiku nina idea yangu hebu ngoja niingie studio nidumbukize hii sauti pengine kesho itanifaa. Na kweli unakaa unapata idea nzuri na unatengeneza kitu kizuri.”
Previous Post Next Post