D’Banj kulishtaki gazeti la ‘Daily Mail’ la Uingereza kwa kumuita ‘Womaniser’

Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kuwa staa wa Naija D’Banj ana uhusiano na muigizaji na model wa Marekani Kenya Moore, habari iliyoandikwa na mitandao mbalimbali likiwemo gazeti la Uingereza ‘Daily Mail’.


D,Banj na Kenya Moore

Kwa mujibu wa mtandao wa 360 Nobs wa Naija, inadaiwa kuwa gazeti hilo liliiandika habari hiyo kwa kumkashifu D’Banj kwa kumuita “Womaniser”, kitu ambacho hakikumpendeza Koko Master hivyo ametishia kulishtaki. Wominiser ni mwanaume ambaye anapenda kuwa na wanawake wengi na kuwa na mahusiano nao ya kimapenzi ya muda mfupi.

D’Banj amesema story kuhusu yeye na Kenya ilikuwa ni uvumi tu, hivyo yuko katika mazungumzo na wanasheria wake kulishitaki Daily Mail.

“It is a rumour. The story has no substance. I’m even about going to sue UK daily mail for the defamation of character. I’m discussing with my legal team. They didn’t hear from me.”

D’Banj ambaye pia ameshirikishwa na star wa Tanzania Diamond Platnumz katika wimbo mpya aliongeza,

“Kila kitu walichoandika ni makosa kabisa. Wamemtafsiri Koko Msater vibaya. Nadhani walitaka kumzungumzia Kenya Moore, ambaye alikuwa Miss America wa zamani, lakini hawakupata ukweli juu ya taarifa yao. Kila kitu walichoandika ni uongo…. They are going to hear from my legal team, soon.”
Previous Post Next Post