Queen Darleen kuzindua video yake mpya April 6 – Club Bilicanas

Queen DARLEEN ambaye pia ni dada wa staa, Diamond Platnumz anatarajia kuionesha video ya wimbo wake “WANATETEMEKA” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake Jumapili hii, tarehe 6 April, 2014 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas.

''
Kwa mujibu wa watu walioiona vide hiyo iliyoandaliwa kwa kiwango kikubwa, wamedai inategemewa kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya video za muziki wa Bongo Flava hasa kwa ubunifu wake na kiwango kikubwa cha picha yenyewe kwa muonekano. Kwenye video hiyo wamo wasanii SHILOLE na DIAMOND PLATNUMZ ikiwa na maana kuwa kwa mara ya kwanza Kaka na Dada (QUEEN na DIAMOND) watokea kwenye video moja ambayo imetengenezwa hapa hapa nchini Tanzania na muandaaji wa video hiyo akiwa ni JERRY MUSHALA.

Wasanii watakaompa kampani QUEEN DARLEEN siku ya uzinduzi ni pamoja na WAKAZI, BARNABA, MWASITI, AMINI,ASIA,NASRY, VJ PENNY, RECHO, CINDY RULZ, PIMP SITTA, HERO pamoja na wasanii Bongo movies wakiwemo WOLPER, RADO na wengine kibao kwenye RED CARPET.

Source:Bongo5
Previous Post Next Post