Mzungu Kichaa amponda Alikiba kwa kudai kuwa alidanganya angelipwa milioni 100 kufanya show Ujerumani

Kati ya vitu ambavyo husaidia kuongeza thamani ya msanii katika macho ya mashabiki ni pamoja na watu kuona akipata dili kubwa na kulipwa pesa nyingi katika shows.


Lakini kumekuwepo baadhi ya wasanii ambao wakati mwingine hutengeneza mazingira ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii, na wengine hata kufanya na Interviews ili tu kufanya watu waamini kuwa thamani yao pia iko juu.

Mzungu Kichaa yuko tofauti kidogo katika hilo, sababu haoni sababu ya msanii kudanganya kwa kitu ambacho sio kweli. Msanii huyo wa Denmark aliyeishi Tanzania kwa miaka mingi alizunguzungumzia swala hilo katika kipindi cha Sporah.



“Mimi siwezi kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema ooh nimetengeneza milioni 100 kwenye show halafu media zote ziseme ‘oooh wow’…kama alivyofanya Alikiba kipindi fulani” Alisema Mzungu Kichaa. “Alisema alikuwa anataka kwenda kufanya show Ujerumani, na alikuja kusema ameahirisha kwenda, tena aliahirisha siku moja kabla, na kusema kuwa angelipwa shilingi milioni 100…Kwahiyo akadai kwamba alikuwa anapewa hiyo hela lakini mikataba haikwenda kama ilivyotakiwa so aliahirisha show siku moja kabla, na kama mwanamuziki mimi najua jinsi mambo ambavyo hua yanakuwa, siamini watu waliokuwa tayari kumlipa kiasi cha pesa kama hicho…na kwa wao kutafuta media publicity kupretend we are getting big money to perform nadhani hilo ni kosa.” Alimaliza.

Crdit:Bongo5
Previous Post Next Post