Mtanzania huyu azitamani Tuzo za Oscar,Kupitia Bongo Movies

Yule aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema anaweza kufanya filamu kama akitokea mtayarishaji atakayeweza kumlipa vizuri na kwamba ana ndoto ya kuchukua tuzo ya Oscar.


Akizungumza na katika kipindi cha maskani cha Time FM jana ,Nando amesema kwa jinsi alivyoowaona watu wa filamu wa Tanzania anahisi inalipa.

“Kama maisha ya bongo movies ndio hivi na mimi nataka bongo movie,lakini mnilipe vizuri tu,nina ndoto za kushinda Oscar,lakini ki East Africa kuna mwanamke kashashinda ya kwanza, always inaniuma, Lakini ndoto hizo zipo, nataka kufanya movie kama zile za akina Fox, kwaHiyo ndoto zipo kibao tu.”

Wakati huo huo ndando amedai kushindwa kufanya kazi na baadhi ya watu kwakuwa hawana uwezo wa kumlipa.

Ammy Nando

“Ukikataa kufanya kazi na watu ambao wanataka ubepari,sijui ana boti nini, mimi ni Mtanzania niliyetika kwenye familia maskini sanaaa, kwamba nimelala nje na mbwa sana yaani masikini sana sanaa na pia nimetokea kwenye famila yenye magari sitini, sabini na Helikopta yaani alitamani hata kununua ndege, baba yangu alikuwa kila kitu lakini ndio nimekulia hapo. Kwahiyo kama unaendesha Porsche,Land Rover, it’s nothing nishaendesha,nimeshapanda, mauncle zetu wanazo maaunt zetu wanazo, sisi ni ma family friend.Ninapo kataa kufanya kazi na wewe I have my duties kwasababu naweza nikaacha kazi yangu na kufanya yako wakati haina maslahi kwangu. Mwisho wa siku utanitapeli,kama nilivyotapeliwa Bilicanas, watu wanajua kama nimelipwa Bilicanas hawajui,nimefanya show pale nimeenda nimezungumza nao hawajanipa pesa mpaka leo,watu mia tano themanini na tano (585) birthday partY ambayo nimesimama dakika ishirini tu,” alisema.

Nando alimalizia kusema kuwa kwa sasa yupo huru kwa kampuni yoyote itakayomuhitaji kibiashara.

Previous Post Next Post