Msanii mkongwe Mr Nice amepata ajali jana akiwa ndani ya bajaji akiwa na abiria mwenzake ndani ya bajaji hiyo. Jinsi ajali hiyo ilivyotokea kuna gari ‘liliwachomekea’ na dereva wa Bajaji hiyo akaamua kuikwepesha na kugonga mti.
Mr Nice akiwa kaumia vibaya usoni |
Hali ya Mr Nice sio nzuri sana,kwani amevimba kichwa na kuumia sana sehemu za usoni na abiria mwenzake ambaye hajafahamika jina alifariki papo hapo na dereva wa bajaji hali yake sio nzuri. Chanzo cha ajali hiyo huenda ikawa ni mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam