Polisi watoa Idadi Ya Waliofariki Dar Kutokana na mvua

Mvua zinazonyesha hivi sasa jijini Dar es salaam zimesababisha uharibifu wa miundombinu, barabara,madaraja na kusimamisha shughuli nyingi za maendeleo kwenye maeneo tofauti.



 Polisi wanasema mpaka sasa watu kumi wamepoteza maisha kwa mua hizi. Watu na familia zao wanaoishi maeneo ya mabonde wamehama na kuacha makazi yao huku vitu vya thamani vikiharibiwa na maji ya mvua.

Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesema wananchi wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.
Previous Post Next Post