Jay Z na mke wake Beyonce kufanya ziara za kimuziki pamoja kuanzia June 2014

Baba na mama Blue ivvy waamua kufanya ziara moja! Patakuwa hapatoshi. Kwa mujibu wa ripoti, wanandoa hao na wazazi wa Blue Ivy watakuwa na ziara ya Marekani.



Tovuti ya Page Six umeandika kuwa wapenzi hao wenye nguvu duniani wapo mbioni kutangaza ziara ya viwanjani ambapo watatumbuiza pamoja kwenye viwanja vikubwa 20 nchini Marekani. Wakati ambapo bado tarehe rasmi ya ziara hiyo haijatangazwa, inadaiwa kuwa inaweza kuanza June na huenda wakawa na show jijini New York, July 4.

Wawili hao wameliza ziara zao binafsi hivi karibuni ambapo Jay Z alimalizia ziara ya show 52 ya ‘Magna Carta…Holy Grail’ mwezi January, wakati Beyonce akimaliza yake ya ‘Mrs. Carter Show’ mwezi March.
Previous Post Next Post

Popular Items