Msanii mkongwe wa Hip Hop, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya, amekanusha kuhusika katika tukio la kumkata mama yake mkumbwa sikio kama ilivyoripotiwa na mdogo wake wiki hii na kudai kuwa yeye ni mtu anayeitambua dini yake.
Dudu Baya amesema baada ya kuzagaa kwa taarifa ya kutafutwa na polisi wa Mwanza kutokana na tuhuma za kumkata mama yake mkubwa sikio: "Unajua hata mimi nashangazwa na hizi taarifa za kutatanisha,mimi Godfrey Tumaini nimesomea dini sana,natambua kipi kibaya na kizuri,siwezi fanya tendo kama hilo kwa mama yangu mkubwa hata siku moja. Unajua sisi ukoo wetu tuna matatizo sana inawezekana kafanya mtu mwingine ila sio mimi.Mimi hapa juzi kati nilipigiwa simu na ndugu zangu pamoja na mama yangu wakaniambia mama yako mkubwa ameKatwa sikio, kwahiyo nashangaa hawa ndugu ambao wameongea kuhusu mimi kumkata sikio mama yangu mkubwa. Jamani mimi siwezi fanya kitu kama hicho. Kwanza sijaonanane muda mrefu sana.”