Al Ahly ya Misri, imebanduliwa nje ya mchuano wa mwaka huu.

Firauni hao ambao wamenyakua kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mara nane, waliyaaga mashindano hayo baada ya kutitimwa mabao matatu kwa mawili (3-2) na somo wao timu ya Libya Al Ahli Bengahzi.

Al Ahli Bengazi iliyofananishwa na daudi, ilijifurukuta na kumwangusha goliathi licha ya kuwa imekuwa ikilazimika kucheza mechi za nyumbani katika nchi jirani ya Tunisia kwa sababu ya ukosefu wa usalama nchini Libya.




Tp Mazembe yafuzu


Al Ahly ya Misri ilikuwa imepoteza mechi ya mkondo wa kwanza 1-0, bao hilo la pekee lilitiwa kimiani na Edward Sadomba.

Ajabu ni kwamba wapinzani wa al Ahly ya Misri Zamalek ilifuzu kwa mkondo ujao baada ya kuilaza Nkana kutoka Zambia kwa mabao matano kwa nunge.

Mabao ya Zamalek yalifungwa na Ahmed Tawfiq, Moemen Zakaria, Omar Gaber, Hazem Emam na Ahmed Gaafar.

Vigogo wengine wa soka ya Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa timu ya kwanza kufuzu kwa hatua ya maondoano baada ya kuilaza Sewe San Pedro ya Ivory Coast mabao 1-0.

Mbwana Ally Samatta ndiye aliyefunga bao hilo la ushindi.

mshambulizi huyo kutoka bongo alikuwa mwiba katika safu san Pedro kwani ndiye aliyeifungia TP Mazembe bao la ungenini majuma mawili yaliyopita huko Abidjan.

Na kwa Mara ya kwanza DRC itakuwa na timu ya pili katika hatua hiyo baada ya Vita Club kuilaza Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini jumla ya mabao 3-0 huko Kinshasa.

Vital ilikuwa imeshindwa 0-2 huko soweto Afrika Kusini Katika mkondo wa Kwanza.

Katika mtokeo mengine ,Sfaxien ya Tunisia ilifuzu baada ya kuilaza Horoya kutoka Guineans 2-0.



Entente Setif ya Algeria ikaibana Coton Sport,ya Cameroonians 1-0 (2-0) nayo Esperance ya Tunisia ikasonga mbele baada ya kuinyeshea a Real Bamako ya mali mabao 3-0.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA