Wema Sepetu: “Kweli niko na Nasib na nadhani muda huu kutakuwa na utulivu ndani yake,”

Mwanadada na Ceo wa Endless Fame Wema Sepetu amethibitisha kuwa kwa sasa yeye na Diamond Platnumz wana uhusiano imara wa kimapenzi ukilinganisha na zamani.



Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, leo, Wema amesema kuwa mapenzi yake na Diamond yamekuwa na nguvu kutokana na kudumu kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka 4.

“Kweli niko na Nasib na nadhani muda huu kutakuwa na utulivu ndani yake,” amesema. “Ule utoto tuliokuwa tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwahiyo tuna ni miaka 4 sasa. Kwa sasa tumeamua kuwa serious.”

Je wewe unaonjae kuhusu wema Sepetu Kurudiana na Diamond Platnumz?
Previous Post Next Post

Popular Items