Victoria Kimani kufanya wimbo na Ommy Dimpoz, adai anaipenda zaidi 'Me and You' kwa Tanzania


wana Omary Nyembo aka Ommy Dimpoz ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania ambao wameyagusa masikio ya mwimbaji wa Chocolate City, Victoria Kimani na kumuweka kwenye orodha ya wasanii wa Tanzania anaowapenda sana.



Vicotia Kimani aliiambia  Times Fm kuwa wimbo Ommy Dimpoz aliomshirikisha Vanessa Mdee ‘Me and You’ ndio wimbo anaoupenda zaidi kwa nyimbo za Tanzania alizozisikiliza.

Tulipotaka kufahamu wasanii wa Tanzania ambao amepanga kushirikiana nao kwenye nyimbo mbali na AY aliyefanya nae Whoa, aliwataja Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee.

“Vanessa Mdee, ningependa kufanya nae kazi na Ommy Dimpoz pia nataka kushirikiana nae pia. Yameshaanza kufanyiwa kazi tayari.” Alisema Victoria.

Tayari ameshafanya wimbo na Vanessa Mdee, kwa hiyo collabo inayofuata itakuwa ya Ommy Dimpoz kwa mujibu wa maelezo yake.

Previous Post Next Post