Kim Kardashian apata ajali ya gari akiwa anaendesha

Mwanamitindo ambaye ni mchumba wa Kanye West, Kim Kardashian jana (March 11) alipata ajali ya gari ambayo haikuwa na madhara makubwa wakati akiendesha gari lake aina ya Mercedes G Wagon na kukwaruzana na Nissan Sentra.



Hata hivyo, gari la Kim Kardashian halikuharibika zaidi mkwaruzo mdogo iliupata lakini Nissan Sentra inadaiwa kuharibika vibaya sehemu ya mbele.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia TMZ kuwa Kim Kardashian alikuwa anakata kona kuelekea kushoto wakati dereva wa gari aina ya Nissan alikuwa anaonesha ishara ya kuelekea kulia, lakini kwa bahati mbaya badala ya kulekea kulia alinyooka na barabara na kulifikia gari la Kim K na kusababisha magari hayo kukwaruzana.



Imeelezwa kuwa wawili hao waliendesha hadi Beverly Hills Hotel ambapo walizungumza na kuyamaliza na kila mmoja akaendelea na safari yake bila polisi kuhusika.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA