Picha: Kwanini Diamond anampenda Wema lakini ndugu zake bado wapo upande wa Penny!

Hakuna ubishi kuwa Diamond Platnumz na Wema Sepetu wanapendana kiasi ambacho hata greda haliwezi kuwatengenisha kwa sasa lakini kuna kitu hakipo sawa.



Ndugu peke wa hitmaker huyo wa ‘My Number One’ aliye karibu naye ni Romy Jones ambaye ni binamu yake lakini wengine wote wapo upande wa mpenzi wake wa zamani, Penniel Mungilwa aka VJ Penny.


Wema akiwa na Romy
Hiyo ina maana kuwa Wema anaweza kuwa ameshinda vita na kuuchukua moyo wa Diamond lakini Penny ameshinda vita kwa kuichukua mioyo ya mawifi zake.. Nani mshindi zaidi hapo?
 Penny, Esma, Halima Kimwana na Wolper

Kuna tetesi pia kuwa hata mama yake bado anamkubali zaidi Penny kuliko Wema. Ni lini umewahi kuona Wema amepiga picha na mama yake Diamond? So mtu pekee wa kumtetea Wema kwa sasa ni Romy na hiyo ina maana kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa anamweka kwenye himaya yake hata ikiwa kwa kutumia fedha.


Penny akiwa na dada zake Diamond wakiwemo Queen Darleen, Esma na Halima Kimwana
Dada zake Diamond, Esma, Queen Darleen na Halima Kimwana, wote wako upande wa Penny. Vyanzo vinadai kuwa Esma na Penny wapo karibu kiasi ambacho wakati mwingine huishi pamoja


Kufanya uhusiano wa Diamond na Wema kuwa wa matata zaidi ni kuwa hata mama yake Wema naye hamkubali Diamond na siku zote humchukulia kama mtu anayemharibu binti yake. Lakini wanasema mapenzi ni kipofu so kwa sasa tuwaache walale.
Previous Post Next Post

Popular Items