Pancho Latino kuizungumzia B'Hitz na yaliyojiri hivi karibuni, ni kwenye THE PLAYLIST ya Times Fm

Mtayarishaji wa muziki wa studio za B’Hitz, Pancho Latino, Jumapili hii atakuwa katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kinachoendeshwa na Omary Tambwe aka Lil Ommy.



Kwa mujibu wa Lil Ommy, Pancho atazungumzia mikakati ya B’Hitz na yale yaliyojiri katika kipindi cha hivi karibuni. Mbali na hayo atazicheza nyimbo tano anazozipenda zaidi.

Kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kinakuwa hewani kila Jumapili kuanzia saa kumi kamili hadi saa kumi na moja jioni.
Previous Post Next Post