Audio: Pancho Latino aizungumzia B'Hitz na yaliyojiri, "mtu kujitoa B'Hitz hakunipunguzii chochote" ampa MRap baraka zote

Mtayarishaji wa muziki wa B’Hitz Music Group, Pancho Latino Jumapili (March 23) alikuwa kwenye kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Omary Tambwe na akazungumzia mengi yaliyojiri hivi karibuni yanayoihusu B’Hitz.



Pancho alijibu maswali kadhaa ikiwa ni siku kadhaa baada ya rapper MRap kuondolewa kwenye label hiyo na kufuata nyayo za wasanii wengine wanne waliondolewa mwaka jana.

Baada ya MRap kuondoka, B’Hitz iliachia nyimbo mbili mpya za MRap huku rapper huyo akiachia wimbo mmoja akiwa nje ya label hiyo.

Pancho alieleza kuwa sababu za B’Hitz kutoa nyimbo hizo ni kutokana na nyimbo hizo kuwa kwenye ratiba ya kutoka hata kabla MRap hajaondoka na kwamba wataendelea na ratiba yao kama kampuni kwa kuwa bado walikuwa na mkataba nae.



“Kila kampuni ina mipango yake kama kampuni ya muziki ya B’Hitz, na hiyo mipango ikishapangwa hatumfuatishi msanii anataka nini. Kwa sababu mara ya kwanza wakati wanakuja huwa tunakubaliana vitu vya kufanya. Kwa hiyo ukiona ngoma kama hizi ambazo zipo kuna mipangilio ambayo tunakuwa tumeshapanga kwamba ngoma fulani itatoka tarehe fulani.

“Kwa hiyo kupishana na MRap kuhusu biashara na kuondoka B’Hitz hakutuharibii sisi mipango ya kuachia sisi ngoma zetu ambazo tulikuwa tumeshaplan kuwa tutaachia.” Amesema Pancho.

Ameeleza kuwa kwa kuwa walikuwa wameshapanga kabla hajaondoka kuwa wataachia nyimbo hizo mbili (Nishike Feat. Rashid na Only You Feat. Jux) na wameendelea na mpango wao huo na kwamba bado wataendelea kutoa nyimbo kama ratiba yao inavyosema.

Pancho amedai kuwa hakuna msanii wa B’Hitz aliyemaliza mkataba wake kama alivyodai MRap kuwa mkataba wake uliisha, isipokuwa msanii mmoja tu aliyeomba kwa maandishi aachiwe na kampuni hiyo.

Alieleza pia sababu zilizowapelekea wasanii hao kuondoka wakati mikataba yao haijaisha na B’Hitz kuamua kuwaacha huru.

“Ni kupishana kibiashara, mnavyopishana kibiashara unajua kila mtu ana ambition zake kama binadamu. Lakini tukija kwenye masuala ya muziki wote tunakuwa na ambition moja.

“Sisi nafikiri ni tatizo letu B’Hitz kutaka muziki wetu ulipe baadae sana. Tumejisahau kwamba wasanii wetu ambao tunadeal nao wanataka muziki wao ulipe kesho…yaani wakitoa track leo kesho apate show. Kwa hiyo hapo ndipo tunapopishana. Tunavyokuwa sisi tunasubira mwenzetu anakuwa na haraka kwa sababu anakaa na watu wanamwambia ‘wewe sikiliza nataka nyimbo mpya hapa nataka show na nini na nini. Ndio hapo tunapopishana sisi, na tunapopishana ndio heshima inakuwa hamna tunakuwa hatuheshimiani ndio kazi inaishia hapo kwa sababu kazi inahitaji heshima.” Ameeleza Pancho Latino.

Ameongeza kuwa wasanii huenda kwake mwanzoni wakiwa wadogo lakini baada ya kuanza kufanya kazi wanakuwa wakubwa na kutaka wasipangiwe kama zamani.

“Akishaanza kupata shows, ukitaka kugombana na msanii wa Tanzania anza kumpangiapangia halafu dai chako. Hapo lazima mvurugane.”

Mtayarishaji huyo wa muziki ameeleza kuwa mambo kama hayo yanatokea pia kwenye studio nyingi ama label nyingi za muziki Tanzania lakini B’Hitz imeangaliwa zaidi na watu.

“Hivi vitu vimetokea na kwingine lakini nashangaa kwa nini watu wameishikia bango B’Hitz..B’Hitz. Nadhani pia ni kwa sababu tulikuwa na powerful team, kwa sababu sisi ndio tulikuwa na team nzuri ambayo imecover kila sehemu. Kulikuwa na Lady singer mzuri Vanessa, kulikuwa na Gosby, kuna MRap, kuna Mabeste, Deddy kuna Dj Choka. Wasanii walikuwa wameshakaa wote.

“Kwa namna moja au nyingine navyosoma comments za mafans facebook wanasema B’Hitz imeisha, lakini kiukweli B’Hitz haijaisha. Kwa sababu sisi wakati tunaanza hii label hatukuwahi kurekodi na upcoming artist, tulivyoanza hii kampuni tulianza kufanya na wasanii ambao wameshafahamika. Ila tukachange hiyo cycle ya kutoka kwenye kufahamika tuinue hivi vipaji vipya kwa sababu tulikuwa na target tofauti, kwa sababu wote tulikuwa tunaona wanaambition kama ya kwetu.” Amesema Pancho.

Alipoulizwa kama anajutia baada ya timu aliyokuwa nayo B’Hitz kuondoka, timu ambayo ameitaja kama timu bora zaidi:



“Si-regret…kwa sababu wote wanaokuja kwangu mimi ndio nawasaidia japo wao wanaandika mistari yao lakini wanatumia beat zangu. Hamna msanii ambaye ameshalipa bili ya umeme, tunasaidiana as binadamu as brothers. Kwa hiyo unapokuja kurekodi kwangu, nakurekodisha bure unatumia beat yangu bure hutoi hata shilingi mia na still unapata shows sipati hata shilingi mia. Mungu mwenyewe anajua shahidi, mtu yeyote msanii aje hapa aseme lini kapiga show kanipa hata shilingi mia. Wanapata show still tunaangalia hizo hela wanaenda nazo wenyewe. Halafu baadae wanarudi wananiongelea vibaya.

Sawa, sikatai..mwisho wa siku mimi umekuja kwangu kuniomba msaada mimi nimekusaidia. Studio time, umeme na nini vitu ambavyo huwezi kuaford kulipa. Kwa hiyo unapokuwa hauwezi kuaford kulipa siku ambayo ukiondoka ukaenda kurekodi sehemu nyingine sijapungukiwa kitu kwa sababu still ulikuwa mzigo kwangu mimi.”

Pancho amedai kuwa hajawahi kupata pesa ya show kutoka kwa msanii yeyote wa B’Hitz zaidi ya shilingi 40,000 aliyopewa na MRap baada ya kufanya show na kulipwa zaidi ya 500,000/-.



Hata hivyo Pancho amemsifia MRap kuwa mbali na matatizo ya kibiashara kati yao, ni rapper mzuri na yuko humble.

“Ni dogo ambaye anafocus ya maisha na anajua anachokifanya pia kwa sababu kupishana kibiashara siwezi kusema nimuongelee vibaya kivyovyote. Ni mtu ambaye anafocus yake na kila mtu ana focus yake kwa hiyo siwezi kumuongelea chochote tofauti ya hapo kwa sababu kila mtu ana destiny yake na kuna mipango Mungu kampangia.

“Kwa hiyo kutoka B’Hitz inawezekana ni njia ya kumfungulia njia nyingine akaendelea zaidi ya hapo, huwezi jua. But ana all my blessings, vyote vilivyopita hapo vimeshapita mimi waga sifikiriagi hivyo vitu.” Alieleza Pancho kabla hajachagua wimbo wa ‘Nishike’ aliofanya MRap na kumshirikisha Rashid.



Previous Post Next Post