MTV Africa Music Awards (MAMA) kufanyika Afrika Kusini kwa mara ya kwanza

MTV Africa Music Awards kwa ufupi MAMA, zimepangwa kufanyika Afrika Kusini kwa mara ya kwanza tangu zianzishwe rasmi mwaka 2008 zilipoandaliwa kwa ushirikiano wa MTV na VIMN (Viacom International Media Networks Africa).


“Tunafurahia kwamba MTV Africa Music Awards 2014 itafanyika kwa mara ya kwanza Afrika Kusini.” Amesema Alex Okosi, makamu wa raisi na mkurugenzi mtendaji wa VIMN Africa.

Tuzo hizo zimepangwa kufanyika June 7, mwaka huu jijini Durban katika ukumbi wa Durban International Convention Centre na zitaoneshwa kupitia MTV Base (DStv 322) na MTV (DStv 130).

Tuzo hizo zimelenga katika kusherehekea muziki wa vijana wa kisasa wa Afrika kama vile Bongo Flava, Dance Hall, Hip Hop, R&B, Afro Pop na nyingine.

Kwa mujibu wa waandaaji, video zitakazoshindanishwa ni zile zilizotolewa kuanzia March 20, 2013 na March 19, 2013.
Previous Post Next Post