Diamond Platnumz kuuza ‘Number 1 Remix’ kama muito wa simu, Ni baada ya kuingia mkataba na MTN Nigeria

Msanii anyehit Bongo na Ngoma Kibao alizonazo Diamond Platnumz ambaye ameondoka usiku wa kuamkia jana kuelekea Nigeria amesema kuwa baada ya Number 1 Remix aliyomshirikisha Davido kutoka, alipokea maombi mengi kutoka kwa makampuni mbalimbali ya simu ya Nigeria wakitaka kumpa dili ya mkataba wa kuuza wimbo huo kama muito wa simu (RBT/Callertune).

Diamond Platnumz akihojiwa Nchini Nigeria katika Redio za The Beat Fm

“Kama wiki ya tatu nilivyotoa tu nikaanza kupokea mikataba tofauti tofauti kutoka Nigeria kuwa kwenye callertune, Ringtone na kadhalika so nikasaini nao vizuri” Alisema PLatnumz.

Akiongea na Millard Ayo kupitia Top 20 ya Clouds Fm, Diamond amesema aliamua kusaini na kampuni ya simu ya MTN na kuwapa Exclusive ili apate pesa nyingi zaidi.

“So Inshallah pia naweza nikarudi na visenti vyangu ambavyo nilisaini…nilisaini na MTN peke yake kwasababu nilitaka kuwapa exclusive ili nipate pesa zaidi”.

‘Number 1′ (original) pia ilimpa dili nono Diamond hapa nyumbani ya kusaini Exclusive na Vodacom Tanzania ili kuuza kama muito wa simu Tanzania mara baada ya kutoka mwaka jana.








Previous Post Next Post

Popular Items