Ccm yashinda Ubunge katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa,

Chama cha Mapinduzi, CCM kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa ameibuka mshindi baada ya kuwabwaga wapinzani wake kutoka vyama vya CHADEMA na CHAUSTA.



Godfrey Mgimwa amepata kura 22,962 akifuatiwa kwa mbali na mgombea Grace Mvanda wa CHADEMA aliyepata kura 5,853 na Alois Minja wa Chama cha CHAUSTA aliyepata kura 150.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga Dr.William Mgimwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania kufariki dunia.

Katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika hivi karibuni katika Kata 27 nchini Tanzania,CCM ilipata viti 24 na wapinzani wao wakubwa CHADEMA waliambulia viti vitatu.
Previous Post Next Post