Bayern Munich watwaa Ubingwa wa ligi kuu ya Bundesliga

Klabu ya Bayern Munich imetwaa taji la ligi kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga kwa kuweka rekodi baada ya kuifunga Hertha Berlin mabao 3-1 usiku wa kuamkia hii leo mjini Berlin.
Shukrani kwao, Toni Kroos, Mario Goetze na Franck Ribery waliofunga mabao hayo na kuwapa ubingwa Bayern zikiwa zimebaki mechi saba ligi kumalizika.



Washindi hao wa mataji matatu msimu uliopita, wamenyakua taji lao la 23 la Bundesliga tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 1963 kwa rekodi ya kushinda michezo 10 mfululizo.
Hiyo inafanya Bayern Munich inayofundishwa na kocha Pep Guardiola ifikishe mechi 19 jumla za kushinda mfululilizo katika mashindano yoet na mechi 52 za ligi kucheza bila kufungwa.
Previous Post Next Post