Unasumbuliwa na tatizo la upweke, Soma hapa

Kutambua umuhimu wa kujifunza ni jambo kubwa lenye thamani katika maisha ya binadamu. Anayejifunza kila siku huongeza maarifa. Hatakuwa vilevile! Huo ndiyo ukweli.


Hapa kwenye Love & Life ndiyo sehemu sahihi zaidi ya kujifunza kuhusu maisha ya ndoa, uhusiano kwa jumla na mengine yanayofanana na hayo. Ndoa ni fumbo. Kabla ya kuingia, lazima upate muda wa kujifunza mambo kadhaa ili yakusaidie.
Ukiingia ukiwa mgeni wa kila kitu, huwezi kufurahia maisha. Marafiki zangu, leo nitazungumzia juu ya kuweza kuushinda upweke katika moyo wako.
Natambua kuna baadhi ya wanawake au wanaume wanakaa kipindi kirefu bila ya kutamkiwa kuwa wanapedwa; kutokana na hali hiyo wanakuwa wapweke na wakati mwingine kufikiria kuwa wao ni wabaya na wasiostahili kabisa kuwa na wapenzi.
Wengine huanza kujiona hawafai kutokana na sababu ambazo wenyewe wataziweka ambazo kwa kiasi kikubwa huwa za kujikosoa!
Wakati mwingine huanza kufikiria kuwa huenda kwa sababu yupo katika hali fulani ndiyo maana hapati mtu wa kumpenda na fikra nyingine mbaya juu yake ambazo huwa ni za kujikatisha tamaa.
Tambua kitu kimoja, kuna wasichana warembo na wavulana watanashati wengi ambao hawajapata pumziko la kweli katika mioyo yao kwa muda mrefu sasa, wamekuwa wakitafuta watu wenye mapenzi ya kweli kwa muda mrefu bila mafanikio na sasa wamekata tamaa ya kupata wapenzi wa kweli na badala yake wamegeuka vyombo vya starehe.


Wavulana watanashati au wasichana warembo mara nyingi watu wa upande wa pili huwatamani zaidi kuliko kuwa na mapenzi ya kweli, kwa maana hiyo baada ya kushiriki naye ngono mara kadhaa huamua kuachana naye na kumuacha muhusika akiwa na sononeko katika moyo wake.Watu
wa aina hii huachwa na dhiki ya moyo na wakati mwingine hukata tamaa na kuamua kutokuwa na uhusiano mwingine kabisa na wapenzi wapya. Jaribu kufikiri kama kuna mtu wa aina hii ambaye amekuwa akitoneshwa mara kadhaa na wapenzi na wewe ambaye una miezi karibu sita sasa hujapata akupendaye nani mwenye matatizo zaidi? Nadhani jibu yakinifu utakuwa nalo.
Inawezekana wewe ni mmoja kati ya hao ambao wana sononeko la moyo kwa kutopata faraja ya kweli kwa wapenzi wao. Hakika hizi ni mada mbili tofauti lakini leo nitaanza na hili la kutopata mpenzi kwa muda mrefu na sasa umekata tamaa ya kupedwa, kuoa au kuolewa katika siku zote za maisha yako. Inawezekana hujafaham
u chanzo cha wewe kutopata mpenzi, lakini kuna mambo mengi ya kuzingatia ili uweze kupata mpenzi na hivyo kuepuka upweke katika moyo wako. Tuendelee kujifunza...
KWANZA UNAJIJALI?
Inawezekana ukawa na maswali lukuki kutokana na ninavyouliza, unajijali? Nataka utambue kitu kimoja, kuwa kuna baadhi ya watu hawajipendi! Hivi unadhani kama wewe mwenyewe hujipendi, hujithamini, nani atakayekupenda?
Ninaposema ujipende namaanisha ujipe upendo ule wa kawaida wewe mwenyewe kabla ya kuhitaji upendo wa mtu mwingine. Mwingine anaweza akawa anavaa nguo chafu, hapigi pasi, nywele zipo timtimu nani atakupenda kwa misingi hiyo?
Hakuna anayependa kuwa na mtu ambaye hana desturi ya usafi. Hata kama ni mzuri kiasi gani unapokuwa upo rafu sana hakuna mtu ambaye atausumbua moyo wake kuanza eti kukufikiria wewe usiyejipenda.
Previous Post Next Post

Popular Items