Pipi apata mtoto wa kiume, ni mtoto wa pili na anaitwa Brandon

Msanii aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Njia Panda, Pipi Doreen,Katika siku ya  jana February 2, 2014 amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa pili wa kiume katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.Na Kuamua kumpa mtoto huyo Jina la Brandon.


Cheek ujumbe aliombatanisha Pipi katika post yake ya instagram


Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Facebook February 2 2014 pipi amepost picha ya mtoto huyo ikiwa na ujumbe huu katika picha: Nina furaha mpaka sijui nisemeje maana naweza nikaandika essay hapa lakini kwa ufupi tu…namshukuru mungu kwa kunipa nguvu…uhai…na mume wangu kipenzi kwa kunipa ujasiri wa kuleta jembe la pili…Asset kubwa kuliko zote duniani asikwambie mtu!!! Welcome to the family baby Brandon !!
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA