Mandela ameacha Mali ya Dola milioni 4.1.Kugawanywa hivi...

Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1. Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.


Mandela alifariki mwezi Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95

Jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.

Jaji alisema kuwa baadhi ya mali hiyo itagawanywa katika wakfu tatu za Mandela ikiwemo moja ya familia yake ambayo itawafadhili zaidi ya watoto na wajukuu 30 wa Mandela pamoja na vitukuu wake.

Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.

Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.

Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.

Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom''

Baadhi ya mali nyingine za hayati Mandela ni nyumba ya kifahari mjini Johannesburg na nyumba nyingine katika kijiji alikozaliwa Eastern Cape.


Source:BBC
Previous Post Next Post