Wimbo wa Jennifer Lopez na Pitpull wachaguliwa kuwa wimbo maalum wa kombe la dunia 2014

FIFA na Sony Music umeutaja wimbo wa Pitbull “We Are One” aliomshirikisha Jennifer Lopez na mwanamuziki wa Brazil, Claudia Leitte kama wimbo rasmi wa kombe la dunia mwaka 2014 June 12 huko Sao Paulo, Brazil.



Wimbo huo utazinduliwa na Sony miezi kadhaa ijayo na utaimbwa siku ya ufunguzi wa kombe la dunia. Video ya “We Are One (Ole Ola)” inafanyiwa kazi.


 Claudia Leitte


“Ninaamini kuwa mchezo huu mkubwa na nguvu ya muziki utatusaidia kutuunganisha” Pitbull alisema jana wakati wa kutangazwa kwa habari hiyo kwenye uwanja wa Macarena, Rio de Janeiro.

Wimbo rasmi wa mwaka 2010 wa FIFA World Cup ulikuwa ni “Waka Waka” ulioimbwa na Shakira na kundi la Freshly Ground la Afrika Kusini.

Previous Post Next Post