Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo.(HM)
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi Waziri alikiri kufuatia taarifa ya CAG kutoa taarifa ya kuwa hoi kifedha.
"Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo."
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na ofisi yake kufanyiwa kazi.

Chanzo: mwanachi
Tags:
Social