Wataalamu waeleza madhara ya Kutumia Internet Mpaka Ikapitiliza

Wafanyakazi wanaojituma kwa kuendelea kufanya kazi kwenye computer zao hata baada ya masaa ya kazi ili kumalizia shughuli zao wanaweza kuwa na mafanikio zaidi lakini wana hatari ya kujikuta wamekuwa na uraibu na internet na kuhatarisha afya zao za akili, imebainika.


Idadi kubwa ya waajiriwa imekuwa ikifanya kazi nje ya ofisi ili kujiongeza kipata na kuborosha career zao lakini kuhatarisha ustawi wao, utafiti mpya umebaini. 

Watafiti katika vyuo viwili vya biashara nchini Uingereza wamesema makampuni yanapuuzia matatizo ya wafanyakazi kuanzisha tabia za uraibu huo kama vile kuamka usiku kuangalia emails, kuwa na wasiwasi wakiwa mbali na computer, sababu walioathirika siku zote huwa waajiriwa bora.

Dr Cristina Quinones-Garcia, wa Northampton Business School, alisema dhana hiyo mpya ya wachapakazi kutumia zaidi mtandao kunaboresha ajira zaidi lakini kuna madhara pia. ‘Watu hao wanaotumia teknolojia kuwasaidia kufanya kazi nje ya masaa ya kazi hufanikiwa zaidi kwenye kazi zao lakini wapo hatarini kuathirika.’
Naye Nada Kakabadse, ambaye ni profesa wa sera, utawala na maadili katika Henley School of Business, alisema wachapakazi hujikuta wakivuka mpaka usionekana na kuanza kutumia internet zaidi ya inavyotakiwa. Muda wa kula na kulala huharibika, uhusiano huathirika na watu huanza kujisikia tofauti wasipotumia computer.

Watafiti hao wanasema waajiri wanatakiwa kuwa na uelewa wa madhara kwa afya ya waajiriwa na wanatakiwa kuweka utaratibu kwao wa jinsi ya kutumia internet nje ya ofisi kwa usalama.

Previous Post Next Post