Mabosi wa Apple na Samsung wakubali kukaa kuzungumzia tofauti zao

Wenyeviti watendaji wa makampuni ya Apple na Samsung wamekubali kukutana pamoja na msuluhishi maalum ili kujaribu kusuluhisha baadhi ya kesi zinazohusiana na kuigana baadhi ya mambo.



Mabosi kutoka kampuni hizo mbili walikutana Jumatatu hii kujadili mambo muhimu katika biashara zao. Majadiliano hayo yamekuja kutokana na amri ya hakimu aliyewataka wakutane kabla ya kesi ya kuchukuliana mifumo na miundo ya simu zao March mwaka huu.

Majadiliano hayo yatafanyika February 19 kukiwa na msuluhishi aliyebobea katika fani hiyo. Hata hivyo majaribio kati ya makampuni hayo kuzungumza ugomvi wao yameshindwa kuzaa matunda. 

Mahakama iliamuru mazungumzo kati ya CEO wa Apple, Tim Cook na mwenzake wa Samsung, Kwon Oh Hyun August 2012 lakini yalishindikana.
Previous Post Next Post