Ray C atoa yake ya Moyoni Baada ya Jack Cliff Kukamatwa na Madawa ya Kulevya Nchini China" Bora Afe tu Mmbwa Mkubwa!"

Hivi karibuni aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva na Radio presenter, mwana dada Rehema Chalamila maarufu kwa jina la Ray C, aliingia katika mjadala mkubwa na mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kupost picha ya mrembo Jackie Cliff aliyekamatwa nchini China kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya jijini Macau nchini humo, na kutoa yake ya moyoni kutokana na tukio hilo.

Picha ikimuonyesha Jack Cliff aliyekamatwa na Madawa ya Kulevya Nchini China 'yako mbele yake" Dec 19/2013

Ray C, aliingia katika mjadala mkubwa na mashabiki wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kupost picha ya mrembo Jackie Cliff Itazame Hapa Chini


Post ya mwana dada Ray C ilizua mjadala mkubwa katika mtandao wa huo wa Instagram kiasi cha kwamba, fans wake walimpa support kutokana na kauli yake ya kutaka Jackie auwawe tu, huku fans wake wengine wakimsihi asimuombe mabaya mrembo huyo aliyekamatwa. Ray C alitoa kauli hiyo kutokana alishawahi kuwa muathirika wa madawa hayo kipindi cha nyuma na kusema kuwa watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu hawana huruma kwa hiyo na yeye hawaonei huruma hata kidogo kwa sababu walimfanya ateseke yeye na familia yake kipindi alipokuwa muathirika wa madawa ya kulevya.

Previous Post Next Post