Maelezo: Hivi ni kweli Ndoa ya Rais wa Marekani Barack Obama na Michelle ipo hatarini?

Wakati ambapo rais wa Ufaransa, Francois Hollande na First Lady, Valerie Trierweiler wanahangaika kuuweka sawa uhusiano wao kufuatia tuhuma za Hollande kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Julie Gayet, ndoa ya rais Barack Obama wa Marekani na Michelle nayo inadaiwa kuwa juu ya mawe.


Yote yalianza kwenye hafla ya kumbukumbu ya Nelson Mandela mwishoni mwa mwaka jana pale ambapo zilisambaa picha zinazomuonesha Michelle akionekana kukerwa na kitendo cha mumewe kupiga picha ya ‘selfie’ na Waziri Mkuu wa Denmark Helle Thorning-Schmidt.




Na kama magazeti ya udaku ya Marekani yanasema ukweli, uhusiano wa wawili hao upo kwenye matatizo makubwa.

Katika kichwa cha habari kisemacho: ‘Obama Divorce Bombshell’, gazeti la National Enquirer linadai kuwa ndoa hiyo yenye miaka 21 imekuwa ikikumbwa na ugomvi wa mara kwa mara ulioanzishwa na tukio hilo kwenye hafla ya kumbukumbu ya Mandela na mbaya zaidi ni kuwa Michelle amegundua kuwa walinzi wa Secret Service wamekuwa wakificha uzinzi unaofanywa na Obama.

Ni madai ambayo ikulu ya White House imegoma kusema chochote.

Gazeti hilo linadai kuwa Mrs Obama, amepanga kuwa pamoja na mumewe hadi atakapomaliza Urais wake ambapo, Obama atarudi Hawaii alikokulia na Michelle atabaki Washington na wanae, Malia na Sasha. Kwa sasa inadaiwa kuwa wawili hao wanalala vyumba tofauti na baada ya Obama kutaka kuweka mambo sawa wakati wa mapumziko yao ya Christmas huko Hawaii, mambo yaligeuka vibaya kiasi cha kumfanya Obama arudi na wanae hao wawili wa kike mjini Washington na kumwacha huko mkewe.


The National Enquirer,lilisema ilipata taarifa hizo kutoka kwa watu wa ndani waliokataa kutajwa majina yao. Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani vimeipuuzia habari hiyo. Hata hivyo kila mmoja anakumbuka jinsi the Enquirer lilivyousema ukweli kuhusu mgombea wa urais wa chama cha Democratic, John Edwards kuwa alizaa na mfanyakazi wa kampeni yake.


Walau gazeti hilo lilikuwa sahihi katika upande mmoja — Ni kweli Mrs Obama alibaki Hawaii. Ikulu ya White House ikatoa maelezo haraka kuwa kuendelea kwake kukaa kulikuwa ni zawadi ya birthday kutoka kwa mumewe.


‘Kama una watoto unajua kuwa kumwambia mwenzi wako kuwa anaweza kukaa wiki mbali na nyumbani ni zawadi kubwa,’ alisema msemaji wa Ikulu.

Tangu Obama achaguliwe kuwa rais, vitabu viwili vilidai kuwa wanandoa hao walikaribia kuachana katika miaka yao ya mwanzo huku Mrs Obama akienda mbali zaidi kwa kuandaa nyaraka za taraka baada ya shughuli zake za siasa kuonekana zinaharibu furaha yao ya nyumbani.


Mwaka 2009, mwandishi wa habari mkongwe wa Marekani, Richard Wolffe alidai kuwa ndoa hiyo kidogo ivunjike miaka tisa iliyopita kutokana na msukomo wa siasa wa Obama na familia yake kuyumba kifedha. ‘Walikuwa wakizungumza kidogo na mapenzi yalipungua,’ aliandika Wolffe.

Kipindi hicho, Mrs Obama alikuwa ametoka kuwa mama— watoto wao Malia na Sasha wana miaka 15 na 12.



Mumewe ambaye walikutana wakati wakifanya kazi kwenye kampuni ya sheria 1989, alikuwa seneta wa Illinois aliyekuwa ameshindwa kwenye uchaguzi wa kiti cha Congress. ‘Alichukia hatua ya kushindwa kwa mumewe kwenye kiti cha Congress mwaka 2000 na ndoa yao iliyumba kipindi binti yao Sasha, alipozaliwa,’ aliandika Wolffe.

First Lady wa zamani wa Ufaransa, Carla Bruni aliandika kwenye kitabu chake kuhusu alivyomuuliza Michelle maisha yalivyo akiwa ikulu kama mke wa Obama. ‘Usiulize! Ni jehanamu. Siwezi kuvumilia!’ Mrs Obama anadaiwa kumwambia Carla. Mrs Obama baadaye alikanusha kuwahi kusema hivyo.

Mwaka 2012, mwandishi wa masuala ya siasa Edward Klein alidai kuwa Obama alikuwa amehuzunishwa mno na kufeli kwa ndoa yake na mwaka 2000 marafiki zake walikuwa na wasiwasi kuwa alikuwa anafikiria kujiua. ‘Michelle alikuwa amechukia kwasababu alimuonya mumewe asigombee uchaguzi wa Congress ambao alishindwa,’ alisema Klein.

‘Wakati wa siku hizo za giza zilizokuja baada ya kushindwa, alirudi kwa Michelle kupata liwazo. Lakini Michelle hakuwa na mood ya kumhurumia,’ aliandika Klein, ambaye alidai kuwa Michelle alifikia hatua ya kuandaa taraka.


Source: Daily Mail
Previous Post Next Post