Hatimaye Alicia Keys Kumaliza Mkataba Wake Na Kampuni Ya Simu Ya Blackberry

Msanii mahiri wa Soul na R&B Alicia Keys anakaribia kumaliza rasmi kutumikia mkataba wake wa mwaka mmoja kama global creative director katika kampuni ya Blackberry smartphones ya Canada mwisho wa mwezi huu. Alicia Keys alilamba dili hilo mapema mwaka jana baada ya kuibuka mshindi katika tuzo za Grammy mapema mwaka jana.


Alcia Keys Kushoto Akisikilza Jambo Kwa Makin jan 30/2013
Moja ya  Picha za Matangazo alizopiga Alicia keys
 Moja ya  Picha za Matangazo alizopiga Alicia keys

Kampuni hiyo Blackberry, imeripoti kuwa ilikuwa na ushirikiano mzuri na imefurahia sana kufanya kazi na msanii huyo mahiri, kampuni hiyo pia imeongeza kuwa inabadilisha mfumo na malengo yake ya kibiashara kutoka kwa wateja wakawaida baada ya kampuni hiyo kushindwa kutamba katika soko hilo na sasa wana malengo ya kujihusisha na mashirika makubwa haswa ya kiserikali na ya kibiashara.


 Alicia Keys Kulia

Previous Post Next Post