Video: Mkalimani wa alama za viziwi kwenye hafla ya kumbukumbu ya Mandela alikuwa ‘feki’

Mkalimani wa alama za viziwi kwenye hafla ya kumbukumbu ya Nelson Mandela amedaiwa kuwa alikuwa feki na ambaye alikuwa akirusha tu mikono kwenye hotuba za viongozi wote walioongea akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama.
Tazama video hapo chini usikie mtaalam wa alama za viziwi akitafsiri alama alizokuwa akizionesha ambazo kwa kawaida alikuwa akiongea pumba tu.

“Ni muongo kabisa, ” Cara Loening, Mkurugenzi wa elimu ya lugha ya alama na maendeleo mjini Cape Town aliliambia shirika la habari la AFP. “Hakuwa anafanya chochote. Hakukuwa na alama yoyote pale. Alikuwa akirusha tu mikono.”

“Jumuiya ya viziwi Afrika Kusini imechukizwa mno na hakuna anayemfahamu mtu huyo,” alisema Loening. “Hatuwezi kupata jina wala kitu chochote. Taasisi iliyopendekeza wakarimani haimjui kabisa.”

Serikali imesema imeanzisha uchunguzi kufuatia madai hayo na matokeo yake yataweka hadharani.

Delphin Hlungwane, msemaji wa shirikisho la viziwi nchini Afrika Kusini alisema mtu huyo alikuwa akirusha tu mikono hewani. “Hakuwa akitafsiri chochote, alikuwa na asilimia sifuri ya ukweli.”

“Watu wa mataifa mengine walikuwa wakiangalia pia na walisema hakuwa anatumia lugha ya alama yoyote. Walisema hawamwelewi,” Hlungwane.
Previous Post Next Post

Popular Items