Mwanamuziki mkongwe wa Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa katika hospitali ya nchini Ubelgiji.
Kwa mujibu wa mwanae Charles Tabu, aliyeongea na Radio Okapi, Tabu Ley amefariki kwa kiharusi na Kisukari.
Naye Nyboma Mwandido, mwanamuziki mwenzie aishiye jijini Paris, Ufaransa amethibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea leo Jumamosi saa 2 asubuhi Brussels. Tabu Ley alikuwa mgonjwa mahututi kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na kiharusi alichokipata mwaka 2008.
Kiharusi (stroke) kilimfanya awe kwenye kiti cha walemavu tangu muda huo. Pamoja na muziki, Tabu Ley aliwahi kuteuliwa kuwa waziri na Rais Laurent Kabila mwaka 1997 na baadaye kuwa mbunge.
Awali, msanii huyo wa Rhumba aliyekataa kuwa mshairi wa Rais Mobutu Sese Seko alilazimika kuikimbia nchi hiyo.
Miaka ya mwishoni alikuwa akiishi Paris, Ufaransa akipata matibabu kabla ya hivi karibuni kupelekwa Ubelgiji kupata matibabu maalum.
Katika miaka 46 ya muziki, Tabu Ley ameshaandika zaidi ya nyimbo 3,000 na kuuza maelefu ya nyimbo.

Tags:
Tragedy