Steps Entertainment yaongelea hali ya soko la filamu ilivyo, yazungumzia pengo la Kanumba

Meneja masoko wa kampuni ya kusambaza filamu nchini, Steps Entertainment Ltd, Ignations D.Kambarage amefunguka kuhusu hali ilivyo katika tasnia ya filamu nchini na kudai kuwa kifo cha Steven Kanumba kilikuwa na athari kubwa.


Meneja Masoko wa Steps Entertainment Kambarage Ignnatus aliyeshika tuzo

“Siku amekufa Kanumba sisi kama Steps tulifunga maduka yetu yote tukapisha kwanza shughuli za mazishi zipite, ila kilichotokea tulianza kuona filamu nyingi za Kanumba mtaani,kumbe kuna watu tayari wameanza kuzidurufisha ili wauze kwa watu ambao wanahitaji kuziona hizo filamu,” alisema.

“Sasa hivi ukitoa filamu leo nchana hapa Dar es salaam,ukipiga simu kesho Arusha na Mwanza wamezipata. Kwahiyo inaonyesha kuna mtandao mkubwa wa hawa watu. Ndio maana wengi tunaowakamata ni matajiri,huku wasanii wenyewe wakilalamika wanaibiwa kumbe sio sisi ni wanaodurufisha kazi zao kungeweza kuwadhibiti labda tungesikia wasanii wakifurahi kupata kinachostahili na kazi wanazofanya,” alielezea.

“Sisi tunachofanya kwa wasanii wao wanaleta story zao, tunazipangia bajeti kwajili wa kuuandaa kazi ya kushoot ,tukimaliza tunampa msanii na director wakafanye kazi. Kwahiyo msanii tumeshakubaliana naye anapewa chake. Kinachobaki ni kumwambia msanii asimamie kazi, akimaliza kazi anatuletea Halafu tunammalizia kiasi kilichobaki.

Msanii wa filamu haibiwi anayeibiwa ni msambazaji, kwasababu msanii anapotupa kazi yake yeye na chake tena kwetu,sisi tunaHitaji kupambana na maharamia wa kazi za wasanii,ambao wakisikia matangazo ya filamu mpya inatarajia kutoka wanajiandaa na empty CD ikitoka tu usiku huo kesho yake tunashangaa kukuta copymbandia mtaani. Kwahiyo sasa hivi tunajitaidi kuendesha kampeni za mara kwa mara kuwakamata hawa maharamia ili na sisi tunufaike.”

Wakati huo huo Kambarage amesema kwa upande wa TRA wamekuwa wakisumbua katika suala stika ambapo anadai mara nyingi wasanii wanakosa stika za kubandika katika kazi zao.

“Kupata Stika TRA kama una filamu ni tatizo sana,mara nyingi ukienda utaambiwa zimeisha na kama zipo wanatulazimisha tununue kwa pesa za kigeni. Wanasema hao jamaa waliopata tenda ya kuzileta wameambiwa wauze kwa pesa kigeni.”

Previous Post Next Post

Popular Items