Star Aliyeng’ara Kwenye Filamu “Captain Phillips” , Barkhad Abdi Kuwania Tuzo za Golden Globe…

Kama wewe ni Mpenzi wa Movie Unaweza Kuwa Umeshaitazam Movie Hii Mpya iliyotoka mwakla 2013 na Hivi ndivyo maisha ya muigizaji huyu ambaye watazamaji wengi wa filamu kutoka sehemu tofauti ulimwenguni imekuwa ni mara yao ya kwanza kumfahamu baada ya kufanya kazi nzuri.


Staa huyu aliyeng’ara kwenye filamu hiyo ya Captain Phillips, Barkhad Abdi hata jina lake hutamkwa kwa utofauti, BARK -ad AHB-dee


Abdi na wenzake kwenye picha ya pamoja..Kikosi cha utekaji nyara “Captain Phillips”

Hiki ni kipande cha cha filamu hiyo ambapo mkali huyu almeigiza kiufasaha..

                                          Tom Hanks(Kushoto) akiwa na Barkhad Abdi

Abdi, ni mzaliwa wa Mogadishu, Somalia, japo alipofikisha umri wa miaka 14, yeye na familia yake walihamia Minneapolis. Alipata elimu yake kwenye chuo cha Minnesota State University, Marekani.

Barkhad, amefanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo hizo za Golden Globe kwenye vipengele vinne kupitia filamu hii ya “Captain Phillips”. Golden Globe, ni tuzo zilizoanzishwa Hollywood, Marekani kwa ajili ya kutambua kazi nzuri za wasanii kwenye filamu na kupitia vipindi vya televisheni, ndani na nje ya marekani. Msimu wa kwanza wa tuzo hizi za Golden Globe, ulifanyika mwaka 1944, kwenye studio za 20th Century Fox, Los Angeles, Marekani.

Kwenye upande wa filamu iliyompa heshima hiyo, Abdi na watekaji nyara wenzie walitumia kipind cha mda wa mwezi mmoja kufanya mazoezi kabla ya kuanza ku-shoot filamu hiyo.

            Barkhad Abdi kwenye moja ya vipande kwenye filamu ya “Captain Phillips”

Akicheza kama kiongozi wa wavamizi toka Somalia na kuiteka meli iliyokuwa ikisafirisha mizigo ya Maersk Alabama na kumteka mkuu msafara wa meli hiyo (captain) ambapo Tom Hanks ndiye aliigiza kwenye nafasi hiyo. Ana uwezo mzuri wa kuzungumza lugha zote mbili, kiingereza na kisomali, ambazo zote zilitumika kwenye filamu hii.

Previous Post Next Post