Picha: Nelson Mandela, Maelfu Waendelea Kuwasili Uwanja Wa FNB Afrika Kusini Tayari Kwa Misa Ya Wafu

Siku ya leo, Disemba 10, ndiyo siku ambayo imepangwa kufanyika misa ya wafu kwa ajili ya kumuombea hayati Nelson Mandela, aliyefarki Disemba 5. Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili ili kuhudhuria misa hii ambayo inafanyika kwenye uwanja mkubwa wa mpira wa miguu, FNB Stadium, Johannesburg ambao ni moja ya viwanja vikubwa vyenye uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 90,000… Mpaka sasa, viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili..

Hapa ndipo hayati Nelson Mandela alipoonekana mara ya mwisho hadharani angali bado yupo hai..
Mmoja wa viongozi wakubwa Duniani wanaotegemewa kuwasili ni pamoja na Raisi wa Marekani, Barack Obama, pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ambaye amekwisha wasili nchini Afrika Kusini…

Hivi ndivyo uwanja huo unavyoonekana kwa sasa ambapo watu wanaendelea kuwasili…

Raisi Jacob Zuma akiwasalimia wageni wengine kabla misa hiyo kuanza muda mfupi ujao..

Raisi Joseph Kabila Wa Congo akiwasili uwanjani hapo…

Source : BBC 
Previous Post Next Post

Popular Items