Siri ya mafanikio makubwa anayoendelea kuyapata Diamond Platnumz, pamoja na kujituma kwake kwa kiwango kikubwa kingine ni jinsi anavyojua kuishi vizuri na watu hasa mashabiki wake wa rika zote.
Diamond akimfariji mtoto aliyeumia wakati akitaka kumuona Diamond pale Leaders siku ya X-mas
Jumatano ya wiki hii (December 25) Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz alifanya show ya Christmas maalum kwa watoto katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es salaam.
Baada ya show yake ya Platnumz alipost picha akimpatia pesa mtoto aliyepata majeraha usoni baada ya kuumia wakati wa show hiyo, alipokuwa akijaribu kutafuta nafasi ya kumuona vizuri msanii huyo ambaye ni kipenzi cha watu wengi, wakubwa kwa wadogo.
Hiki ndicho alichoandika kwenye blog yake This Is Diamond sambamba na picha hizo:
Diamond akimfariji mtoto aliyeumia wakati akitaka kumuona Diamond pale Leaders siku ya X-mas
Jumatano ya wiki hii (December 25) Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz alifanya show ya Christmas maalum kwa watoto katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es salaam.
Hiki ndicho alichoandika kwenye blog yake This Is Diamond sambamba na picha hizo:
“Napenda nitoe pole za dhati kabisa kwa binti huyu mdogo,aliyepata majeraha usoni wakati akijaribu kupata nafasi ya kunishuhudia..yote ni kutokana na msongamano mkubwa wa watu uliokuwepo.. NAWAPENDA MASHABIKI WANGU..NAWAPENDA SANA WATOTO WOTE”.
Source: This is Diamond