Rafiki wa karibu wa video queen maarufu nchini, Jackie Cliff amethibitisha taarifa zinazoendelea kukua kwa sasa kuwa msichana aliyekamatwa na kilo 1.1 ya madawa ya kulevya aina ya Heroin huko Macau, China ni yeye.
Chief Rocka akiwa na girlfriend wake pamoja na Jackie na Jux
Bongo5 imeongea kwa simu na Chief ambaye yupo masomo nchini China kujua undani wa tukio hilo.
“Amekamatwa kweli,” Chief ameiambia Bongo5. “Nlivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akamatwa. Mimi nilijua sababu nilipigia simu watu wa ubalozini baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona au kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo upo Hong Kong wao ndio wakaniambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndo kakamatwa, hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia,” Chief ameeleza.
Chief Rocka akiwa na Jackie
Awali tuliandika kuwa pamoja na jina la mrembo huyo kutajwa na vyanzo vingi kuwa ni kweli amekamatwa, tulichelea kulitaja jina lake ili kuepusha kuandika habari isiyo na uhakika.
Rafiki huyo wa Jackie, ambaye pia ni rafiki mkubwa Jux mwenye uhusiano wa karibu na Jackie, Chief Rocka (kiongozi wa kundi la Rockaz) ameandika kupitia Instagram:
“I feel so sorry for jackie…God be with u and help u thru this one…we r human we make mistakes…wuldnt want to jump on judgin u like how other people do….this is Bad…2013 plz its enuf.”
Bongo5 imeongea kwa simu na Chief ambaye yupo masomo nchini China kujua undani wa tukio hilo.
“Amekamatwa kweli,” Chief ameiambia Bongo5. “Nlivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akamatwa. Mimi nilijua sababu nilipigia simu watu wa ubalozini baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona au kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo upo Hong Kong wao ndio wakaniambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndo kakamatwa, hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia,” Chief ameeleza.
Jackie Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya akiwa amesimama karibu na meza yalipowekwa madawa yaliyotolewa kutoka kwenye mwili wake
Amesema kwakuwa Jackie amekamatwa Macau ambako kuna sheria tofauti na upande wa bara wa China, adhabu yake inaweza kuwa ndogo kuliko ile ya kunyongwa ambayo hutolewa bara.
Jackie Cliff akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa huko Macau
“Inategemea ukimatwa mainland China halafu labda ukamatwa Macau au kwa Macau na Hong Kong ni kama uko kwetu nikama Tanzania na Zanzibar. Kwahiyo yeye alikokamatiwa ni kama yupo Zanzibar ni ndani ya China lakini inajitegemea lakini sheria zake sio kali sana. Lakini sasa mpaka wajaji kutokana na mzigo walioubeba, wengine wanasema miaka mitatu, wengine minne, wengine wanasema wanatoa kama Hong Kong miaka nane so inategemea na akiisaidia polisi akisema watu aliokuwa akiwapelekea mzigo wapi na wakapatikana, I don’t know.”
Inadaiwa kuwa madawa haya yalipatikana mwilini mwa mrembo huyo. Madawa hayo aina ya Heroin yana thamani ya shilingi milioni 85
Amesema kuonana na Jackie kwa sasa sio rahisi kwakuwa wengine wasema uwezekano huo unaweza kupatikana mwezi wa tatu mwakani.
Chief ameongeza kuwa hakuna sehemu mbaya na hatari kukamatwa na madawa ya kulevya kama China.
“Navyosema kwamba I feel sorry for her ni kwasababu mimi nimekuwa hapa miaka mitano at least naongea kichina yaani hata wakikifunga you can socialise with people lakini sasa kwa yeye ambaye haiongei,… yaani ukiweka ubinadamu, ukiachana na hayo mambo sijui ya madawa ya kulevya yule ni msichana ni kama wasichana wengine wowote , yaani kama dada yako au demu wako akikamatwa awekwe ndani kwenye nchi ya ugeni ni jambo kubwa yaani especially kwa mtu ambaye umeshamfahamu kidogo huwezi kuanza kumjudge kisa amepost picha ya Benz yake, yaani she is a hardworking woman. Suala la madawa sio zuri lakini sio kila mtu anaweza akafanya.”
Rapper huyo amesema picha zilisombaa mtandaoni zikimuonesha msichana mwenye koti la njano akiwa amekamatwa ni za Jackie.
“Ametoka kwenye gazeti la China Daily, ni gazeti kubwa, ni yeye,” amesisitiza.Mtandao wa China Daily uliandika: Msichana mwenye miaka 28 kutoka Tanzania alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki madawa ya kulevya huko -Macao, Dec 19, 2013. Alikuwa ameficha kilo 1.1 za heroin zenye thamani ya $137,720 ( sawa na zaidi ya shilingi milioni 85) ndani ya mwili wake na kuchukua ndege kutoka Thailand hadi Macao. Alisema alikuwa akielekea Guangzhou, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa China Guangdong.

Waandishi wa habari wakipiga picha madawa ya kulevya aina ya Heroin yaliyokamatwa pamoja na vitu vingine.
Hizi ni Baadhi ya Video ambazo Mrembo uyu anaonekana..
Msikilize Chief Rocka hapa:
Source:Bongo5
Tags:
celebrity News