MAN U YATAKA KUVUNJA REKODI YA DAU LA USAJILI KUSAJILI KIUNGO DORTMUND

Klabu ya Manchester United imeonywa kwamba mchezaji chaguo la kwanza la David Moyes katika usajili wa dirisha dogo, Marco Reus atawagharimu hadi Pauni Milioni 40 ili kumpata. (HM)

Kiungo Reus ana thamani ya Pauni Milioni 29.4 Borussia Dortmund.

Lakini inafahamika mambo yamebadilika tangu Bayern Munich ionyeshe nia ya kutaka kumsajili Mario Gotze.


Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England watatakiwa kuvunja rekodi yao ya dau la usajili ili kuipata saini ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

Wasaka vipaji wa United wakuwa wakisaka mchezaji wa kiwango cha dunia kwa nafasi yoyote.

Pamoja na hayo, kiungo huyo anabakia kuwa chaguo lao la kwanza, ingawa pia wanasaka na washambuliaji, beki wa kushoto na beki wa kati waje kuwa warithi wa Patrice Evra na Rio Ferdinand mwishoni mwa msimu.
Previous Post Next Post