KUPIGA PICHA YA 'SELFIE' KWA RASI BARACK OBAMA NA WAZIRI MKUU WA DENMARK WAKIWA NA DAVID CAMEROON KWENYE KUMBUKUMBU YA MANDELA KWAKOSLEWA

Mapozi za Rais Barack Obama wa Marekani kwenye tukio la kumbukumbu ya Nelson Mandela jana jijini Johannesburg yametiliwa mashaka.


Obama, waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na waziri mkuu wa Denmark, Minister Helle Thorning-Schmidt wakipozi kujipiga picha

Kwanza, Obama alishikana mikono na Rais wa Cuba, Raul Castro wakati alipokuwa akielekea kwenda kuzungumza mbele ya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa soka wa FNB.

Obama akishikana mkono na Rais wa Cuba

Tukio hilo la muda mfupi, lililonaswa kwenye video na kwenye picha lilizua mjadala wa haraka ambapo Wamarekani walijadili umuhimu wa marais hao kushikana mikono wakati nchi hizo hazina uhusiano mzuri kidiplomasia tangu mwaka 1959.

Seneta John McCain alifananisha tukio hilo kama kushikana mikonona Adolf Hitler.

“Unawezaje kushikana mkono na mtu ambaye anawaweka Wamarekani jela? McCain aliiambia Public Radio International.
Msaidizi wa Obama aliiamboa Yahoo News kuwa tukio hilo halikuwa limepangwa. “Pamoja na yote, leo ni siku ya Nelson Mandela, na hilo ndio lengo moja la Rais.”

Katika tukio jingine, Rais Obama alipozi kuchukua picha ya “selfie” kwenye siti aliyokuwa amekaa pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na waziri mkuu wa Denmark, Minister Helle Thorning-Schmidt. First lady Michelle Obama, aliyekuwa amekaa kushoto kwao hakushiriki kwenye picha hiyo.

“Dear Obama,” mwandishi wa Mashable, Christine Erickson aliandika.”Funerals are no place for selfies.”


Obama na waziri mkuu wa Denmark wakifurahia maongezi huku Michelle akifuatilia kinachoendelea uwanjani hapo




Previous Post Next Post