Kaa tayari Kusikiliza Ngoma Mpya Kutoka Kwa Linex Aliyomshirikisha Ommy Dimpoz Pamoja na Recho

Msanii wa bongo fleva Linex Sunday Mjeda amefanya collabo na wasanii wenzake wanaouwakilisha mkoa wa Kigoma Ommy Dimpoz pamoja na Recho katika wimbo wake mpya aliomaliza kuurekodi jana.

Linex amesema wimbo huo utakuwa ni wa tofauti na nyimbo ambazo zimezoeleka kwa Watanzania na kuongeza kuwa katika wimbo huo mzee wa Tupogo Dimpoz ameimba kwa kuchanganya na lugha ya Kiha.


“Hiyo ngoma jana ndiyo tumemaliza mimi Dimpoz na Recho, imefanywa na Fundi Samweli pamoja na Tudd Thomas na ngoma inaitwa INGO, Ommy kaimba Kiha hatariiii” Amesema Linex.

Akielezea maana ya Ingo, Linex amesema “Ni Kiha na maana yake ni Njoo, but ni neno linalotumika kwa makabila mengi East Africa kama Rwanda, Burundi na UG”.

Katika wimbo huo Linex amesema yeye na Ommy wamegawana verse moja moja, huku chorus akisimama mwenyewe na vionjo vya sauti tamu ya Recho vimepita kwa mbali.

Kuhusu mipango ya video ya wimbo huo Sunday Mjeda aka V.O.A amesema tayari amesaini mkataba na Samaki Samaki ambao ndio watakaosimamia video hiyo.

“Pia nimesaini contract na Samaki Samaki Fleva juzi kwaajili ya kushoot video kubwa, so wao ndiyo watakuwa wasimamizi wa video ya ‘Ingo’.
Linex ameongeza kuwa anatarajia kuutoa wimbo huo January 2014.
Previous Post Next Post