Jokate Mwegelo Azindua Kidoti Club Kuhusika na Maswala ya Urembo

Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 na Mmiliki wa Kidoti  Jokate Mwegelo,  siku ya leo amezindua rasmi Club yake ambayo inaitwa Kidoti Club itakayokuwa ikihusika na maswala ya urembo. Mrembo huyo pia amezindua mitindo mipya ya nywele, ambayo inajuliakana kama Kidoti Brand.


Katika club hiyo ya Kidoti itakua ikijihusisha na maswala ya kutoa ushauri katika jamii ikiwa pamoja na taarifa za kimuziki, filamu na kazi za kisanaa kiujumla kwa kila rika katika jamii, Kidoti Club lengo lake kubwa haswa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na kuwapa nafasi watu wengine waweze kujiunga.


Kiongozi wa club hiyo Miss Mwegelo ambaye ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006,amesema kuwa ili uweze kupata nafasi ya kujiunga na kuwa mwanachama katika clabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678, baada ya hapo utaanza kupata taarifa mbali mbali kuhusiana na Kidoti Club.

Esther Wassira (kulia) akisoma ujumbe mara baada ya kujiunga na Club ya Jokate, katikati ni Jokate na wa kwanza kushoto ni Bhoke wa EATV

“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii. Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake. Mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbalimbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi.

“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji changu kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu nami kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote. Natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya maisha.”

** Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbal mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwaajili ya rika tofauti.**

Previous Post Next Post