Klabu ya Simba jana imefanikiwa kumsajili mlinda mlango wa zamani wa Yanga na Klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Ivo Mapunda kwa mkataba ya miezi 18.
Ivo Mapunda na beki wa kati wa Klabu ya nchini Kenya, Gormahia,Donald Mosoti ni wachezaji wapya wa Simba SC kuanzia jana, ambapo wanatarajia kuonyesha makeke yao msimu ujao katika Klabu hiyo.
Kipa huyo amejipatia umaarufu nchini hapa kwa ushujaa wake wa kupangua mikwaju ya penalti.
Katika mchezo wa jana wa Kombe la Chalenji kutafuta mshindi wa tatu kati ya Zambia (Chipolopolo) na Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Mapunda alidaka penalti mbili kati ya nane ambazo mabingwa hao wa zamani wa Afrika –Chipolopolo walipiga.
Simba imeonyesha kutokuwa na imani na safu yake ya makipa inayoongozwa na Mganda Abel Dhaira baada ya kuamua kumsainisha mkataba wa miezi sita kipa wa zamani wa watani wao wa jadi, Yanga, Mgana Yaw Berko na hapo jana Ivo Mapunda kwa mkataba wa miezi 18.
Kutua kwa Mapunda Simba kutaisaidia timu hiyo iliyopo katika mgogoro mkali wa uongozi kwani kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hakuna timu itakayoruhusiwa kuwa na kipa wa kigeni ili kukidhi matakwa ya Azimio la Bagamoyo.
Kipa Ivo Mapunga akisaini mkataba kuishezea Simba.

Source:Nipashe,
Tags:
Sports