Beckham Apata Dili Nzito, Ni Katika Kuitangaza Kasino

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, David Beckham amesaini mkataba wa kusaidia kuzitangaza casino za Las Vegas Sands’ nchini Singapore Macau.


Sands imesema kwenye maelezo yake kuwa ina matumaini itapata mafanikio kutokana na umaarufu wa Beckham katika maeneo hayo. Kampuni hiyo yenye makazi yake jijini Las Vegas lina casino kubwa zaidi huko Macau, kitovu cha michezo ya kamari ya kisasa duniani.

Mkataba huo unaweza kusaidia Sands kuvutia biashara hiyo huko China, ambako biashara ya casino ni haramu na matangazo yake yanapigwa marufuku. Soka ni mchezo maarufu zaidi China.





Previous Post Next Post